NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE 2026 – MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (NAFASI 04)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe anawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kuwasilisha maombi ya kazi kwa ajili ya kujaza nafasi nne (04) za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II, kama ilivyoelezwa katika tangazo hili.
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 04
1.1 Kazi na Majukumu
Mwombaji atakayefaulu kuajiriwa atawajibika kutekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni, kuwahoji kuhusu mahitaji yao na kuwaelekeza katika ofisi au sehemu husika kwa ajili ya kupata huduma.
- Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba nyingine za kazi.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kuyasambaza kwa Maafisa katika Idara, Vitengo au Sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada na nyaraka katika sehemu zake.
- Kupanga dondoo za vikao na kufanya maandalizi ya mikutano mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
1.2 Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na kuwa na cheti cha mtihani husika.
- Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 katika fani ya Uhazili kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa kasi ya maneno 100 kwa dakika moja.
- Awe amepata mafunzo ya kompyuta na kuwa na ujuzi wa kutumia programu za ofisi kama Microsoft Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.
1.3 Ngazi ya Mshahara
Mshahara utalipwa kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali vya TGS C.
2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
Waombaji wote wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo:
- Waombaji wote wawe raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45, isipokuwa wale ambao tayari wako kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi. Wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu walionao katika Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote wanapaswa kuambatisha Wasifu Binafsi (Detailed Curriculum Vitae – CV) ulio na taarifa kamili, anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana, anuani ya barua pepe pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba na wanapaswa kuzingatia maelekezo yaliyomo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria au Wakili. Vyeti vinavyotakiwa ni pamoja na:
- Vyeti vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita, kwa wale waliofikia viwango hivyo.
- Vyeti vya Stashahada, Shahada, Stashahada ya Juu na Elimu ya Uzamili, pale inapohusika.
- Vyeti vya mafunzo ya kompyuta.
- Vyeti vya taaluma kutoka katika bodi husika zinazotambuliwa.
- Hati zifuatazo hazitakubaliwa:
- Testimonial.
- Provisional Results.
- Statement of Results.
- Hati za matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (Results Slips).
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika, zikiwemo TCU, NECTA na NACTE.
- Waombaji waliostaafishwa au kuondolewa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wawe na kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji watakaobainika kuwasilisha taarifa au vyeti vya kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Novemba, 2026.
2.1 Anwani ya Barua ya Maombi
Kila mwombaji anatakiwa kuambatisha barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na nakala za vyeti vyake vya elimu na taaluma.
Barua hiyo ielekezwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE,
S.L.P 28001,
KISARAWE.
2.2 Namna ya Kutuma Maombi
Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kupitia anuani ifuatayo:
Mfumo huo pia unapatikana kupitia tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kuchagua sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal.
MUHIMU: Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
3.0 TAREHE YA MWISHO WA MAOMBI
<text>20 NOVEMBA, 2026</text>
Waombaji wanashauriwa kuhakikisha wanawasilisha maombi yao mapema na kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika kabla ya tarehe ya mwisho.
TANGAZO LIMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE.