Nafasi za kazi za Walimu Jiji La Mwanza November 2026 TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA MFUPI – HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza anawatangazia Watanzania wenye sifa zinazotakiwa kuomba nafasi za kazi za muda mfupi kama ifuatavyo:
1. WAKUSANYA MAPATO (REVENUE COLLECTORS) – NAFASI 40
2. WALIMU DARAJA LA III B – NAFASI 12
Masomo yanayohitajika:
-
Hisabati – nafasi 2
-
Sayansi – nafasi 3
-
Lugha na Sanaa – nafasi 7
3. MWALIMU DARAJA LA III C (SAYANSI NA HISABATI) – NAFASI 3
SIFA MUHIMU ZA WAOMBAJI
A. Sifa za Wakusanya Mapato
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
-
Awe raia wa Tanzania.
-
Awe na elimu ya Kidato cha Nne (CSEE) na kuendelea.
-
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta au simu janja.
-
Awe na uwezo wa kufanya hesabu na kutunza kumbukumbu za fedha.
-
Awe mwaminifu, mchapa kazi na mwenye kujituma.
-
Awe mkazi wa Wilaya ya Nyamagana.
B. Sifa za Walimu
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
-
Awe raia wa Tanzania.
-
Awe na cheti cha Kidato cha Nne au Kidato cha Sita.
-
Awe na Stashahada ya Ualimu (Diploma in Education) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
Kwa nafasi za Mwalimu Daraja la III C (Sayansi na Hisabati):
– Awe na Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Elimu yenye masomo ya Sayansi na Hisabati.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wote wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo:
-
Kuandika barua ya maombi ya kazi.
-
Kuambatisha nakala za vyeti vya Elimu na Taaluma.
-
Kuambatisha nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.
-
Kuambatisha wasifu binafsi (CV), wadhamini wawili (2) pamoja na picha za passport za hivi karibuni.
ANUANI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yawasilishwe kwa anuani ifuatayo:
MKURUGENZI,
HALMASHAURI YA JIJI,
S.L.P 1333,
MWANZA.
TAREHE YA MWISHO YA MAOMBI
13 NOVEMBA 2026
SAA 9:30 ALASIRI
ANGALIZO: Waombaji wanashauriwa kuhakikisha kuwa maombi yao yanawasilishwa kabla ya muda wa mwisho uliotajwa.
Tangazo la Nafasi za Kazi za Muda Mfupi – Halmashauri ya Jiji la Mwanza.