Matokeo ya Darasa la Saba 2026
Matokeo ya Darasa la Saba 2026
 Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (Primary School Leaving Examination – PSLE) husimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ambalo lina jukumu la kutathmini maarifa na ujuzi walioupata wanafunzi katika kipindi chao cha elimu ya msingi.
 Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2026 Kupitia NECTA
Baada ya NECTA kutangaza matokeo, wanafunzi na wazazi wataweza kuyaangalia kupitia tovuti rasmi kwa kufuata hatua hizi:
- Fungua kivinjari cha intaneti kwenye simu au kompyuta yako.
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kupitia https://www.necta.go.tz.
- Chagua sehemu ya Results.
- Fungua kipengele cha PSLE – Primary School Leaving Examination.
- Chagua mwaka wa mtihani 2026, mara tu matokeo yatakapowekwa.
- Chagua mkoa ambao mwanafunzi alifanyia mtihani.
- Chagua halmashauri au wilaya husika.
- Tafuta jina la shule aliyosoma mwanafunzi.
- Fungua orodha ya matokeo na tafuta namba ya mtihani ya mwanafunzi husika.
Kiungo Rasmi cha Matokeo ya Darasa la Saba NECTA:
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
PSLE-2026 EXAMINATION RESULTS
Â
BOFYA HAPA KUANGALIA MATOKEOÂ
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2026 kwa Simu (SMS)
NECTA pia ina huduma ya kupata matokeo ya mitihani kupitia simu ya mkononi kwa kutumia mfumo wa USSD.
Ili kutumia huduma hiyo:
- Piga 15200# kwenye simu yako.
- Chagua namba 8 – ELIMU.
- Chagua namba 2 – NECTA.
- Fuata maelekezo yatakayoonekana kwenye simu yako.
Huduma hii inasaidia watumiaji ambao hawana uwezo wa kutumia intaneti. Ada au masharti ya huduma yanaweza kutegemea mtoa huduma wa simu.